Pindi mja atakapokwenda kinyume na Hadiyth ambazo ni Swahiyh na ziko wazi kwa ajili ya kufata matamanio au kumfuata kichwa mchunga mmoja katika watu, basi humthubutikia ghadhabu na hasira za Mola. Aidha kuna khatari moyo wake kupinda na kupewa mtihani. Allaah (Subhaanah) ameonya jambo hilo pale aliposema:

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Basi watahadhari wale wanaokwenda kinyume amri yake; isije kuwapata fitina au ikawapata adhabu iumizayo.”[1]

فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ

“Pindi walipopotoka, basi Allaah akazipotosha nyoyo zao. Na Allaah haongoi watu mafasiki.”[2]

فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ

“Basi akawapachika unafiki katika nyoyo zao mpaka siku watakayokutana Naye kwa vile walivyomkhalifu kwao Allaah kwa waliyomuahidi na kwa yale waliyokuwa wakikadhibisha.”[3]

[1] 24:63

[2] 61:5

[3] 09:77

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jawaab al-Mufiyd fiy Hukm-it-Taswwiyr kutoka katika Majmuu´-ul-Fataawaa (04/218)
  • Imechapishwa: 28/03/2022