Imaam ´Abdul-Ghaniy bin ´Abdil-Waahid al-Maqdisiy (Rahimahu Allaah) amesema:

200 – ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiku ukija hapa – yaani mashariki – na ukaondoka mchana hapa – yaani magharibi – na likazama jua, basi amekwishafungua mfungaji.”[1]

Imekuja katika tamko jengine:

“Usiku ukija hapa – yaani mashariki – na ukaondoka mchana hapa – yaani magharibi – na likazama jua na jua likazama, basi amekwishafungua mfungaji .”

Hata kama bado kutakuwa mwangaza na umanjano duniani havingatiwi. Muda wa kuwa jua limeshazama amekwishafungua mfungaji. Haijalishi kitu ile athari za umanjano kwenye milima na kwenye miti muda wa kuwa jua limezama basi amekwishafungua mfungaji. Lakini ikiwa halijazama isipokuwa tu limezuiwa na mlima, nyumba au kitu kingine basi asifungue mpaka pale atakapojua kuwa limekwishazama. Hapo ni pale ambapo litapotea upande wa magharibi. Jua likishazama basi amekwishafungua mfungaji hata kama kutakuwa kumebaki athari ya mwanga upande wa kando ya mlima au manjano upande wa ncha ya miti. Umanjano hayo ni mwanzo wa usiku. Mambo haya hayazingatiwi. Muhimu jua liwe limeshazama. Ikishazama diski ya jua basi amekwishafungua mwenye kufunga.

[1] al-Bukhaariy (1954) na Muslim (1100).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ifhaam fiy Sharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/411-412)
  • Imechapishwa: 23/03/2022