07. Hadiyth ”Je, hampangi safu sawa zenu kama wanavyopanga safu sawa Malaika mbele ya Mola wao?”

20 – Jaabir bin Samurah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijitokeza kwetu na kusema:

”Je, hampangi safu sawa zenu kama wanavyopanga safu sawa Malaika mbele ya Mola wao?” Tukasema: ”Ee Mtume wa Allaah, vipi Malaika wanavyopanga safu mbele ya Mola wao? Akasema: ”Wanazikamilisha safu za mbele na wanakaa sawa katika safu.”[1]

[1] Muslim (340) na Ibn Hibbaan (2159) kwa ukaguzi wa al-Albaaniy.

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ujuwb Taswiyat-is-Sufuuf
  • Imechapishwa: 22/01/2025