237 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´an) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

الإمام ضامنٌ والمؤذن مؤتمَن، اللهم أرشِد الأئمةَ واغْفِرْ للمؤذِّنين

“Imamu ni mdhamini[1] na muadhini ameaminiwa[2]. Ee Allaah! Waongoze maimamu na wasamehe waadhini.”[3]

Ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy. Imekuja kwa Ibn Khuzaymah och Ibn Hibbaan:

“Allaah akawaongoza maimamu na akawasamehe waadhini.”[4]

Ibn Khuzaymah ana upokezi kama wa Abu Daawuud. Imekuja katika mwingine:

“Waadhini wameaminiwa na maimamu ni wadhamini. Ee Allaah! Wasamehe waadhini na watengeneza maimamu.”

Alisema hivo mara tatu.[5]

238 – Ameipokea pia Ahmad kupitia kwa Abu Umaamah kwa cheni ya wapokezi nzuri[6].

[1] Bi maana amepewa jukumu la swalah za waswaliji.

[2] Bi maana amepewa jukumu la nyakati za swalah.

[3] Swahiyh.

[4] Swahiyh.

[5] Swahiyh.

[6] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/214)
  • Imechapishwa: 23/02/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy