Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Na sharti zake ni kumi:
1 – Uislamu.
2 – Kuwa na akili.
3 – Kuweza kupambanua.
4 – Nia.
5 – Mtu asinuie kuukata [wudhuu´ wake] mpaka atakapomaliza kutawadha.
6 – Kukatika kwa yale yanayowajibisha wudhuu´.
7 – Kujisafisha kwa maji au kwa kutumia mawe kabla yake.
8 – Maji yawe masafi na yenye kuruhusiwa/ya halali.
09 – Kuondosha kila kinachozuia maji kufika kwenye ngozi.
10 – Kuingia kwa wakati wa kile kitendo cha faradhi kwa yule ambaye daima yuko katika hali ya hadathi.
MAELEZO
Tayari tumeshazungumza kuhusu masharti ya Uislamu, akili na kupambanua. Ama kwa upande wa sharti ya nia, basi mtu anapotia wudhuu´ ananuia moyoni mwake kuondoa hadathi na asitamke kwa ulimi wake. Vivyo hivyo katika ´ibaadah zote mtu ananuia moyoni mwake bila kutamka kwa ulimi, isipokuwa katika Hajj na ´Umrah, ambapo anaruhusiwa kutamka kile alichonuia kwa kusema:
لبيك عمرة
”Nimekuitikia ´Umrah.”
au:
لبيك حجّاً
”Nimekuitikia Hajj.”
au:
لبيك حجّاً وعمرة
”Nimekuitikia Hajj na ´Umrah.”
Iwapo mtu ataosha uso wake baada ya kuamka usingizini pasi na kunuia wudhuu´ kisha akaanza kutawadha, basi ni lazima aoshe uso tena kwa ajili ya wudhuu´, kwani kuoshwa huko kwa kwanza hakutoshi kwa kuwa hakukuwa na nia ya wudhuu´ wakati huo. Ikiwa mtu mwenye janaba ataoga kwa ajili ya kupunguza joto huku amesahau kuwa yuko katika janaba, basi kuoga huko hakutoshi kumwondolea janaba kwa sababu hakuwa na nia ya kuondoa hadathi kubwa. Ikiwa mtu ataambatanisha kuoga huko na twahara, basi hukumu hiyo huendelea mpaka twahara hiyo ikamilike. Ikiwa atakata nia hiyo katikati ya wudhuu´, halafu akataka kukamilisha wudhuu´ wake, haijuzu kwake, bali ni lazima aanze tena wudhuu´ kutoka mwanzo, kwa sababu tayari alikuwa ameifuta sehemu aliyokwishafanya. Hii ndiyo sharti ya tano.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 9-10
- Imechapishwa: 30/04/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 9-10
Imechapishwa: 30/04/2026
https://firqatunnajia.com/06-sharti-za-wudhuu-ni-kumi/