04. Sharti ya tatu ya swalah ni kupambanua

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Sharti ya tatu ni kupambanua (Tamyiyz) na kinyume chake ni utoto. Mpaka wake ni miaka saba. Hapo ndipo ataamrishwa kuswali, kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Waamrisheni watoto wenu kuswali wanapofikisha miaka saba, wapigeni wanapofikisha miaka kumi na watenganishe baina yao katika malazi.”[1]

MAELEZO

Iwapo mtoto mdogo atafikia umri wa kupambanua mambo – ambao ni miaka saba – basi ataamrishwa kuswali, si kwa namna ya wajibu. Wajibu huja baada ya kubaleghe. Kuamrishwa kwake swalah katika umri huu ni ili azoee kuswali na kuitekeleza kwa namna iliyowekwa na Shari´ah.

Anapofikia miaka kumi, basi amri ya swalah inasisitizwa zaidi juu yake na kutiwa adabu kwa kipigo kisichoumiweza. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Waamrisheni watoto wenu kuswali wanapofikisha miaka saba… ”

Hii ni Hadiyth Swahiyh aliyopokea Ahmad (6756, 6689) na Abu Daawuud (495) kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Aidha ameipokea Abu Daawuud (494) kupitia kwa Sabrah bin Ma´bad al-Juhaniy (Radhiya Allaahu ´anh). Tazama ”Irwaa’-ul-Ghaliyl (247).

[1] Abu Daawuud (495) na Ahmad (6756). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (1/266).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 6-7
  • Imechapishwa: 30/04/2026

Turn on/off menu