Sharti ya pili ni kuwa na akili na kinyume chake ni wendawazimu. Mwendawazimu kalamu yake imesimamishwa mpaka anapopata akili. Dalili ni Hadiyth:
“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu; aliyelala mpaka anapoamka, mtoto mpaka anapobaleghe na mwendawazimu mpaka anapopata akili.”[1]
MAELEZO
Ni lazima kwa anayeswali ndani ya swalah yake awe na akili timamu, si mpotevu wa akili kwa sababu ya wazimu au ulevi. Mwendawazimu kalamu imenyanyuliwa kwake, si mwenye kubebeshwa jukumu. Mlevi, ambaye amejipotezea akili, amefananishwa na wendawazimu na kwa sababu haelewi swalah yake.
Shaykh (Rahimahu Allaah) ametoa dalili kwa Hadiyth ya:
“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu… ”
Ni Hadiyth Swahiyh ambayo ameipokea Abu Daawuud (4398), an-Nasaa’iy (3432) na Ibn Maajah (2041) kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Tazama ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (297) cha al-Albaaniy.
[1] Abu Daawuud (4405) na Ahmad (1362). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2/5).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 5-6
Sharti ya pili ni kuwa na akili na kinyume chake ni wendawazimu. Mwendawazimu kalamu yake imesimamishwa mpaka anapopata akili. Dalili ni Hadiyth:
“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu; aliyelala mpaka anapoamka, mtoto mpaka anapobaleghe na mwendawazimu mpaka anapopata akili.”[1]
MAELEZO
Ni lazima kwa anayeswali ndani ya swalah yake awe na akili timamu, si mpotevu wa akili kwa sababu ya wazimu au ulevi. Mwendawazimu kalamu imenyanyuliwa kwake, si mwenye kubebeshwa jukumu. Mlevi, ambaye amejipotezea akili, amefananishwa na wendawazimu na kwa sababu haelewi swalah yake.
Shaykh (Rahimahu Allaah) ametoa dalili kwa Hadiyth ya:
“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu… ”
Ni Hadiyth Swahiyh ambayo ameipokea Abu Daawuud (4398), an-Nasaa’iy (3432) na Ibn Maajah (2041) kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Tazama ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (297) cha al-Albaaniy.
[1] Abu Daawuud (4405) na Ahmad (1362). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2/5).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 5-6
https://firqatunnajia.com/03-sharti-ya-pili-ya-swalah-ni-akili/