Swali 06: Tunawasikia watu wengi wakitamka nia kwa sauti wakati wanapoingia ndani ya swalah. Ni ipi hukumu? Je, ni kitu kina msingi katika Shari´ah?
Jibu: Hakuna msingi wa kutamka kwa sauti nia katika Shari´ah takasifu. Ni kitu hakikuhifadhiwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum) kutamka nia kwa sauti wakati wanapoingia ndani ya swalah. Hakika si venginevyo nia mahali pake ni moyoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika si venginevyo matendo yanategemea nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa kiongozi wa waumini ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 07
- Imechapishwa: 09/08/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Hakuna haja ya kutamka nia kwa sauti wakati wa kutawadha
Swali: Ni ipi hukumu ya kutamka nia katika swalah na katika wudhuu´? Jibu: Hukumu ya hilo ni kwamba ni Bid´ah. Kwa sababu haikunakiliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah zake. Kwa hiyo ni lazima kuliacha. Nia mahali pake ni moyoni. Kwa hivyo hakuna haja…
In "Wudhuu´"
Kutamka nia kwa sauti
Swali: Ni ipi hukumu ya kutamka kwa sauti nia ya swalah? Jibu: Kutamka nia ni Bid´ah. Kuidhihirisha kwa sauti ni dhambi zaidi. Sunnah ni kunuia kwa moyo. Kwani Allaah (Subhaanah) anajua siri na yaliyojificha. Yeye ndiye kasema: قُلْ أَتُعَلِّمُونَ اللَّـهَ بِدِينِكُمْ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ”Sema:…
In "Nia ya swalah"
Hukumu ya kutamka nia ya kutawadha
Swali: Nikinuia ndani ya msikiti kwa kusema kwa mfano: اللهم إني نويت الوضوء لصلاة العصر “Ee Allaah! Hakika mimi nanuia wudhuu´ kwa ajili ya kuswali swalah ya ´Aswr.” au nikanuia kuswali kwa njia kama hii – je, kunazingatiwa ni Bid´ah? Jibu: Kutamka nia, si ndani ya swalah wala katika wudhuu´, …
In "Nia ya swalah"