06. Nia ya swalah haitamkwi kwa sauti

Swali 06: Tunawasikia watu wengi wakitamka nia kwa sauti wakati wanapoingia ndani ya swalah. Ni ipi hukumu? Je, ni kitu kina msingi katika Shari´ah?

Jibu: Hakuna msingi wa kutamka kwa sauti nia katika Shari´ah takasifu. Ni kitu hakikuhifadhiwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum) kutamka nia kwa sauti wakati wanapoingia ndani ya swalah. Hakika si venginevyo nia mahali pake ni moyoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika si venginevyo matendo yanategemea nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa kiongozi wa waumini ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 07
  • Imechapishwa: 09/08/2022