05. Amebainikiwa kuwa ameswali kinyume na Qiblah

Swali 05: Ni ipi hukumu ikibainika kuwa swalah imeswaliwa kinyume na Qiblah baada ya kujitahidi? Je, kuna tofauti ikiwa hayo yametokea katika nchi ambayo sio ya waislamu, nchi ya makafiri au ikawa mwituni?

Jibu: Muislamu akiwa safarini au katika mji ambao asimpate ambaye atamwelekeza katika Qiblah, basi swalah yake ni sahihi ikiwa atajitahidi kukilenga Qiblah kisha baadaye ikabainika kuwa ameswali kinyume chake. Lakini akiwa katika mji wa waislamu, basi swalah yake si sahihi. Kwa sababu alikuwa na uwezo wa kumuuliza wa kumwelekeza Qiblah. Ni kama ambavo alikuwa na uwezo wa kujua Qiblah kilipo kupitia misikiti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 06-07
  • Imechapishwa: 09/08/2022