04. Kanzu fupi lakini mavazi mengine chini ya kongo mbili za miguu

Swali 04: Tunawaona baadhi ya watu wanafupisha kanzu zao na wanarefusha suruwali zao. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Sunnah ni mavazi yao yawe kati ya nusu muundi mpaka kwenye kongo mbili za miguu. Haijuzu kuteremsha chini ya kongo mbili za miguu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kile chenye kuvuka chini ya macho mawili ya mguu katika kikoi basi kiko Motoni.”

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

Hapana tofauti kati ya suruwali, kikoi, kanzu na juba. Hakika si venginevyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametaja kikoi kwa njia ya kupigia mfano na si kwa njia ya kwamba ni kikoi peke yake. Bora ni mavazi yawe mpaka kwenye kongo mbili za miguu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kikoi cha muumini ni mpaka kwenye nusu ya muundi.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 05-06
  • Imechapishwa: 09/08/2022