06. Kumuomba Allaah unachotaka mwishoni mwa Tashahhud

36 – ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafunza Tashahhud kisha akasema mwishoni mwake:

“Kisha akachague du´aa itayompendeza na aombe kwayo.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

Imekuja katika tamko la Muslim:

“Kisha achague katika maombi anayotaka.”

MAELEZO

Hadiyth inafahamisha kuwa aombe mahitaji mbalimbali ya Aakhirah na dunia. Hata hivyo aanze kwa du´aa zilizopokelewa ingawa hapana vibaya akiomba du´aa ambazo hazikupokelewa, kwa sababu watu wana haja mbalimbali. Kwa hiyo inajuzu kuomba du´aa ya mali ya halali, mke mwema, nyumba nzuri, kunusuriwa kutokana na dhuluma na mfano wa hayo.

[1] al-Bukhaariy (835) na Muslim (402).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 40
  • Imechapishwa: 08/10/2025