05. Saa ambayo mtu anaitikiwa maombi yake siku ya ijumaa

35 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitaja siku ya ijumaa kisha akasema:

“Humo mna saa ambayo hakuna muislamu anayeafikiana nayo huku anaswali akimuomba Allaah kitu, isipokuwa humpa nacho” akaashiria kwa mkono wake kuonyesha udogo wake.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

MAELEZO

Hadiyth inajulisha kuwa siku ya ijumaa kuna saa ya kuitikiwa. Allaah ameificha saa hii na hakuibainisha, kama ilivyotangulia ya kwamba usiku pia kuna saa ya kuitikiwa ambayo Allaah ameificha. Hilo ni kutokana na hekima kubwa. Nayo – ijapo Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwa sababu mja aweze kujitahidi kuitafuta mchana mzima wa siku ya ijumaa na katika usiku mzima kwa nisba ya saa ya usiku.

Haafidhw Ibn Hajar ametaja maoni arobaini kuhusu saa ya kuitikiwa du´aa siku ya ijumaa. Maoni yenye nguvu zaidi katika hayo:

1 – Ni kuanzia pale imamu anapoketi chini mpaka kumalizika kwa swalah.

2 – Zile saa za mwisho za mchana.

[1] al-Bukhaariy (935) na Muslim (852).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 39
  • Imechapishwa: 08/10/2025