06. Hakuna yeyote aliyethibitisha kuwepo kwa waungu wawili wanaolingana

Aina hii ya Tawhiyd [Rubuubiyyah] kama ambavo hakuna kundi katika wanaadamu ambalo liliipinga basi vivyo hivyo mara nyingi hakukutokea shirki ndani yake. Kila mmoja anakiri ya kwamba Allaah amepwekeka kwa uumbaji na uendeshaji wa mambo. Hakukuthibiti kutoka kwa kundi lolote ulimwenguni ambalo lilithibitisha kuwepo kwa waumbaji wawili ambao wako sawa katika sifa na matendo. Washirikina majusi ambao wanaonelea kuwa ulimwengu una waumbaji wawili; muumbaji wa kheri, ambaye ni nuru, na muumbaji wa shari, ambaye ni giza. Lakini hata hivyo hawasawazishi giza na nuru. Wanaona kuwa nuru ndio msingi na dhuluma ni kitu kimejitokeza. Wamekubaliana juu ya kwamba nuru ni bora kuliko giza.

Kadhalika manaswara ambao wana imani ya utatu hawakuuthibitishia ulimwengu kuwepo kwa waungu watatu tofauti. Bali wote wamekubaliana juu ya kwamba Muumbaji wa ulimwengu ni mmoja na wanasema kwamba baba ndiye Mungu mkubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 14
  • Imechapishwa: 21/03/2019