07. Kuamini Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah peke yake haitoshi

Kwa kifupi ni kwamba kuthibitisha Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ni pahali pa maafikiano na shirki ndani yake ni ndogo. Lakini kuikubali yenyewe tu hakumtoshelezi mja na kumwingiza katika Uislamu. Bali ni lazima pamoja na hivyo kuleta kile kinachopelekea: Tawhuyd-ul-Ilaahiyyah.

Nyumati za kikafiri zilikuwa zikikubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na khaswa washirikina wa kiarabu ambao Mtume wa mwisho (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumilizwa kwao. Hilo halikuwafanya kuwa waislamu muda wa kwamba hawakuleta Tawhiyd-ul-Ilaahiyyah.

Mwenye kuzisoma Aayah za Qur-aan ataona kuwa ni zenye kumtaka mtu kuleta Tawhiyd-ul-Ilaahiyyah na inatolewa dalili kwa Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Inawataka washirikina kile walichokanusha na wakati huohuo inatoa dalili dhidi yao kwa kile walichokithibitisha. Kwa msemo mwingine ni kwamba inawaamrisha Tawhiyd-ul-´Ibaadah na inawakhabarisha kule kukiri kwao Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Inataja Tawhiyd-ul-´Ibaadah katika mazingira ya kuwataka waisimamishe na Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah katika mazingira ya kuwaeleza nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 14
  • Imechapishwa: 21/03/2019