742- Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Bwana mmoja alisema: “Ee Mtume wa Allaah! Unasemaje juu mtu ambaye anatolea mali yake zakaah?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Yule mwenye kuitolea mali yake zakaah basi ameondokwa na shari.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Awsatw” na tamko ni lake, Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” yake na al-Haakim kwa mukhtaswari:

“Ukitoa zakaah ya mali yako, basi imekuondoka shari yake.”

Amesema:

“Ni Swahiyh juu ya sharti za Muslim.”

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/457)
  • Imechapishwa: 14/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy