06. Hadiyth “Atakayesema mfano wa anayosema huyu… “

255 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

:كنَّا مع رسولِ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ -، فقام بلالٌ ينادي، فلمَّا سكت، قال رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

.”مَن قال مِثلَ ما قال هذا يقيناً دخل الجنة”

“Tulikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasimama Bilaal kutoa adhaana. Aliponyamaza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Atakayesema mfano wa anayosema huyu hali ya kuwa na yakini, basi ataingia Peponi.”[1]

Ameipokea an-Nasaa’iy, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na al-Haakim ambaye amesema:

“Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/221-222)
  • Imechapishwa: 07/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy