05. Hadiyth “Yule atakayesema wakati wa kumsikia muadhini… “

254 – Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesema wakati wa kumsikia muadhini:

وأنا أشهدُ أن لا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وحدَهُ لا شريكَ لَهُ و أنَّ محمَّدًا عبدُهُ ورسولُهُ رضيتُ باللَّهِ ربًّا وبالإسلامِ دينًا وبمحمَّدٍ رسولا

“Nami nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Naridhia Allaah kuwa Mola wangu, Uislamu kuwa dini yangu na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa Mtume wangu.”

basi atasamehewa dhambi zake.”[1]

Ameipokea Muslim, at-Tirmidhiy na tamko ni lake, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na Abu Daawuud ambaye hana tamko linalosema “…. basi atasamehewa dhambi zake.” Imekuja kwa Muslim:

“… basi atasamehewa dhambi zake zilizotangulia.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/221)
  • Imechapishwa: 07/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy