2 – Miongoni mwa yanayothibitisha kuingia kwa mwezi wa Ramadhaan, ikiwa mwandamo haukuonekana, ni kukamilisha idadi ya Sha´baan siku thelathini. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”… ukifunikwa juu yenu basi kadirieni.”
Maneno Yake:
”… ukifunikwa juu yenu… ”
maana yake ni kwamba ikiwa kitu kitafunika mwandamo kikazuia kuonekana kwake usiku wa tarehe thelathini ya Sha´baan, ni mamoja iwe ni mawingu au vumbi, basi kadirieni idadi ya mwezi wa Sha´baan iwe kamili kwa kuutimiza siku thelathini. Hili linafafanuliwa na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth nyingine:
”Ukifunikwa juu yenu, basi kamilisheni idadi siku thelathini.”[1]
Maana ya hili ni kuharamishwa kufunga siku ya shaka. ´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Atakayefunga siku inayotiwa shaka, basi amemuasi Abul-Qaasim (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[2]
Kwa hiyo ni wajibu kwa muislamu kufuata yaliyokuja kutoka kwa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swawm yake na katika ´ibaadah zake zote. Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wameweka utambuzi wa kuingia kwa mwezi wa Ramadhaan kwa alama mbili zilizo wazi na zinazojulikana kwa mtu wa kawaida na kwa msomi:
1 – Kuuona mwandamo.
2 – Kukamilisha idadi ya Sha´baan siku thelathini.
Atakayekuja na jambo analodai kuwa ndilo linalowajibisha swawm, kinyume na alichokibainisha Muwekaji wa Shari´ah, basi amemuasi Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ameongeza katika aliyoyaweka Allaah na Mtume Wake katika Shari´ah na pia amezua katika dini yasiyokuwa ndani yake. Kila Bid´ah ni upotofu. Mfano wa hilo ni anayesema kuwa ni wajibu kufuata hEsabu za falaki katika kuthibitisha kuingia kwa mwezi wa Ramadhaan, hali ya kuwa hesabu hizo zinakabiliwa na makosa. Isitoshe ni jambo lililofichika lisilojulikana kwa kila mtu[3]. Katika hili kuna uzito na dhiki juu ya ummah. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ
“Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika dini.”[4]
Kwa hiyo lililo la wajibu juu ya waislamu ni kutosheka na yale aliyoyaweka Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Shari´ah, kama ilivyo wajibu juu yao kutosheka na mambo mengine yasiyohusu mwandamo, kushirikiana juu ya wema na kumcha Allaah.
[1] al-Bukhaariy na Muslim.
[2] Abu Daawuud (2334), at-Tirmidhiy (686), an-Nasaa´iy (2190) na Ibn Maajah (1645). Abu ´Iysaa at-Tirmidhiy amesema:
”Nzuri na Swahiyh.”
[3] Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
”Nimewaona watu katika mwezi wao wa swawm na katika miezi mingine pia, miongoni mwao wapo wanaosikiliza yanayosemwa na baadhi ya wajinga wa watu wa hesabu, kwamba mwandamo unaonekana au hauonekani, kisha wanajenga juu ya hilo ama kwa ndani yao au kwa ndani na nje yao, mpaka ikafika kwangu kwamba miongoni mwa baadhi ya mahakimu kulikuwa na anayekataa ushahidi wa idadi ya watu waadilifu kwa kauli ya mhesabu mjinga mwongo anayesema unaonekana au hauonekani, akawa ni miongoni mwa wanaokadhibisha haki ilipowajia… ” Kisha akasema: ”Hakika sisi tunajua vyema kabisa katika dini ya Uislamu kwamba kufanya kazi katika kuonekana kwa mwandamo wa swawm, mwezi wa Hajj, mwezi wa eda, mwezi wa kiapo cha kujiepusha na mahusiano ya ndoa au hukumu nyinginezo zilizounganishwa na mwandamo kwa khabari ya mhesabu kwamba unaonekana au hauonekani, hilo halijuzu. Maandiko mengi yaliyoenea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu hilo ni mengi. Aidha waislamu wameafikiana juu yake na wala haijulikani humo tofauti ya zamani kabisa wala tofauti ya karibuni.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (25/131–132)).
[4] 22:78
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 14-15
- Imechapishwa: 26/01/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 14-15
Imechapishwa: 26/01/2026
https://firqatunnajia.com/05-njia-ya-pili-ya-namna-unavyothibiti-mwezi-wa-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket