Maneno yake (Ta´ala):
لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
“… ili mpate kumcha Allaah.”
Kwa maana kwa sababu ya kufunga. Hivyo basi kufunga kunapelekea kumcha Allaah kwa sababu inaidhibiti nafsi na kuvunja matamanio.
Maneno yake (Ta´ala):
فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ
“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini [akafunga baadhi ya siku], basi [akamilishe] idadi [ya siku anazotakiwa kufunga] katika siku nyinginezo. Na ni juu ya wale wanaoiweza [kufunga swawm] lakini kwa tabu watoe fidia kulisha masikini.”[1]
Imesemwa kuwa ni siku zisizo za Ramadhaan ambazo zilikuwa siku tatu. Vilevile imesemwa kuwa ni siku za Ramadhaan, kwa sababu amezibainisha katika Aayah inayofuata kwa maneno Yake:
شَهْرُ رَمَضَانَ
“Mwezi wa Ramadhaan… “
Wamesema kwamba mwanzoni mwa Uislamu walikuwa wakipewa uchaguzi kati ya swawm na fidia, kwa maneno Yake (Ta´ala):
وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ ۚ وَأَن تَصُومُوا خَيْرٌ لَّكُمْ
“Na ni juu ya wale wanaoiweza [kufunga swawm] lakini kwa tabu watoe fidia kulisha masikini. Na atakayejitolea kwa jema lolote lile basi ni bora kwake, na mkifunga swawm ni bora kwenu.”[2]
Kisha uchaguzi huo ukafutwa kwa kuwajibishwa swawm moja kwa moja kwa maneno Yake (Ta´ala):
فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ
“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi [mpya] na afunge swawm.”[3]
Hekima ya hatua hii ni taratibu katika Shari´ah na kuwahurumia ummah, kwa sababu walipokuwa bado hawajaizoea swawm, kuwajibishwa moja kwa moja kulikuwa na uzito. Kwa hiyo wakapewa uchaguzi mwanzo, kisha walipoimarika yakini yao, nafsi zao zikatulia na wakaizoea swawm ndipo ikawajibika juu yao swawm peke yake. Mfano wa hili upo katika hukumu nyingine nzito za Shari´ah ya Uislamu ambapo huwekwa kwa taratibu. Lakini sahihi ni kwamba Aayah hiyo imefutwa kwa mwenye uwezo wa kufunga. Ama kwa asiyeweza kufunga kwa sababu ya uzee au maradhi yasiyotarajiwa kupona, basi Aayah haikufutwa kwake. Huyo anaruhusiwa kufungua na kulisha chakula masikini mmoja kwa kila siku na wala halazimiki kulipa.
Ama wasiokuwa hao, basi lililo wajibu juu yao ni kufunga. Atakayefungua kwa sababu ya maradhi ya muda au safari, basi ni wajibu juu yake kulipa, kwa maneno ya Allaah (Ta´ala):
فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ
“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au yuko safarini, hivyo basi akamilishe idadi katika siku nyinginezo.”[4]
Swawm ya mwezi wa Ramadhaan ilifaradhishwa katika mwaka wa pili baada ya kuhajiri. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunga Ramadhaan tisa. Swawm ya Ramadhaan ikawa ni wajibu wa lazima na ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu. Atakayekanusha uwajibu wake amekufuru. Atakayefungua bila udhuru huku anakiri kuwa ni wajibu, basi amefanya dhambi kubwa ambaye ni wajibu aadhibiwe na azuiwe na anapaswa kutubu kwa Allaah na kulipa alichokifungua[5].
[1] 02:183-184
[2] 02:184
[3] 02:185
[4] 02:184
[5] Ikiwa sababu ya kufungua kwake ni kufanya tendo la ndoa mchana wa Ramadhaan basi, mbali na kulipa, anapaswa kutoa kafara nzito, kama kutavyokuja ubainifu – Allaah akitaka.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 12
- Imechapishwa: 26/01/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 12
Imechapishwa: 26/01/2026
https://firqatunnajia.com/03-baadhi-ya-faida-katika-aayah-inayofaradhisha-swawm/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket