Allaah (Ta´ala) amesema:
فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ
“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi [mpya] na afunge swawm.”[1]
Allaah (Subhaanah) amewajibisha katika Aayah hii uwajibu juu ya waja Wake wa kufunga mwezi wa Ramadhaan wote kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake. Mwanzo wake hutambuliwa kwa mojawapo ya mambo mawili:
1 – Kuonekana kwa mwandamo wake kutokana na Hadiyth iliyopokelewa na al-Bukhaariy na Muslim na wengineo kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mnapouona mwandamo fungeni na mnapouona basi fungueni. Ukifunikwa juu yenu basi kadirieni.”[2]
Imaam Ahmad na an-Nasaa´iy wamepokea kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Msifunge mpaka muone mwandamo wala msifungue mpaka muone.”[3]
Kwa wawili hao kuna nyongeza ambayo ni ile sentesi ya mwisho katika Hadiyth ya kwanza, nayo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”… ukifunikwa juu yenu basi kadirieni.”
at-Twabaraaniy pia amepokea kupitia kwa Twalq bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza:
”Allaah amefanya miezi yenye miandamo kuwa ni nyakati. Hivyo basi mnapouona fungeni na mnapouona basi fungueni.”[4]
Vilevile al-Haakim amepokea kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye ameeleza:
”Allaah amefanya miezi yenye miandamo kuwa ni nyakati kwa watu. Hivyo basi fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona.”[5]
Katika Hadiyth hizi Tukufu kuna kuhusishwa uwajibu wa kufunga Ramadhaan na kuonekana kwa mwandamo wake na kukatazwa kufunga bila kuuona mwandamo. Vilevile imekuja ya kwamba Allaah amefanya miezi yenye miandamo kuwa ni nyakati kwa watu, kwa kupitia hizo wanajua nyakati za ´ibaadah zao na miamala yao. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ
”Wanakuuliza kuhusu miandamo ya mwezi. Sema: ”Hivyo ni vipimo vya nyakati kwa watu na Hajj.”[6]
Hili ni miongoni mwa rehema za Allaah kwa waja Wake na wepesi Wake juu yao, kwa kuwa amehusisha uwajibu wa swawm na jambo lililo wazi na alama iliyo dhahiri wanayoiona kwa macho yao. Si sharti mwandamo uonekane na watu wote, bali ukionwa na baadhi yao, hata kama ni mtu mmoja tu, basi watu wote wanalazimika kufunga.
Ibn ´Abbaas amesema:
”Alikuja mbedui mmoja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi nimeuona mwandamo.” Kwa maana mwandamo wa Ramadhaan. ”Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Je, unashuhudia kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah?” Akasema: ”Ndiyo.” Akasema: ”Ee Bilaal, watangazie watu wafunge kesho.”[7]
Vilevile imepokelewa kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwamba amesema:
”Watu waliangalia mwandamo ambapo nikamweleza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba nimeuona. Basi akafunga na akawaamrisha watu wafunge.”[8]
[1] 02:185
[2] al-Bukhaariy (1900) na Muslim (08/1080).
[3] al-Bukhaariy (1906) na Muslim (03/1080) na tamko ni la wote wawili hao.
[4] at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (08/397) (nr. 8237).
[5] al-Haakim (01/423), Ahmad (04/23) na ad-Daaraqutwniy (02/163). al-Haakim amesema:
”Swahiyh kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.”
[6] 02:189
[7] Abu Daawuud.
[8] Abu Daawuud (2342).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 12-14
- Imechapishwa: 26/01/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 12-14
Imechapishwa: 26/01/2026
https://firqatunnajia.com/04-njia-ya-kwanza-ya-namna-unavyothibiti-mwezi-wa-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket