05. Maana ya kufikisha kutoka kwa Mtume ijapo Aayah moja

Pengine mtu akauliza kama haya niliyoyasema yanapingana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fikisheni kutoka kwangu ijapokuwa Aayah?”[1]

Hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fikisheni kutoka kwangu… “

Kwa hivyo ni lazima yale tunayoyafikisha yawe kweli yametoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ndio tunayoyakusudia. Tunaposema kuwa ni lazima kwa mlinganizi awe na elimu hatumaanishi kwamba ni lazima awe amebobea ndani ya elimu. Tunachokusudia ni kwamba asilinganie isipokuwa kutokana na yale anayoyajua na wala asizungumze yale asiyoyajua.

[1] al-Bukhaariy (3461).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Zaad Daa´iyah ila Allaah, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 01/11/2021