Usiku wa Qadar umefichwa kwa ummah. Hautambuliki wakati wake kama mfano wa saa ya kuitikiwa du´aa siku ya ijumaa. Allaah anayo hekima kubwa ya kuuficha ili waislamu waweze kuutafuta, hima yao iwe kubwa na uwe na kasi utafutaji wao. Kwa sababu endapo wangelijua ni usiku fulani basi azma ingelipotea mwezi mzima na akafufuka kuutafuta usiku huo peke yake. ´Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kwa ajili ya kutueleza usiku wa Qadar. Wanamme wawili wa kiislamu wakagombama ambapo akasema: “Nimetoka kwa ajili ya kukuelezeni usiku wa Qadar fulani na fulani wakagombana ambapo ukanyanyuliwa. Pengine ikawa ni kheri kwenu. Hivyo basi, utafuteni katika siku ya tisa, siku ya saba na siku ya tano.”[1]

Maana yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… fulani na fulani wakagombana… “

Wakaingia katika mzozo ambao ni ugomvi, matusi na kupandisha sauti, mambo ambayo ni mabaya. Kwa ajili hiyo wakanyimwa baraka za usiku wa Qadar katika usiku huo, kitu ambacho kilitangulia katika ujuzi wa Allaah (Ta´ala). Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kuna faraja ya kile husemwa kwamba magomvi yanakata faida na elimu yenye manufaa. Imepokelewa katika Hadiyth:

“Hakika mja hunyimwa riziki kwa dhambi inayompata.”[2]

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“…ukanyanyuliwa.”

Bi maana ikanyanyuliwa elimu ya nyinyi kulengeshewa na si kwamba ujuzi wake umenyanyuliwa moja kwa moja. Kwa sababu amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya hapo:

“Hivyo basi, utafuteni katika siku ya tisa, siku ya saba na siku ya tano.”

Kwa hivyo ni lazima kwa muislamu kupupia kuhakiki na kuifikia kheri hii kwa kufanya ´ibaadah na utiifu katika nyusiku za kumi la mwisho kama vile kuswali, kusoma Qur-aan, Dhikr, du´aa na kila ayawezayo katika matendo mema yenye kubakia. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] al-Bukhaariy (2023).

[2] Tafsiyr Ibn Kathiyr (08/471).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswar Ahaadiyth-is-Swiyaam, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 03/03/2023