Amesema:

فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ فَلَا أَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلَا يَتَسَاءَلُونَ

”Wakati litakapopulizwa baragumu, basi hakutokuwa na unasaba baina yao Siku hiyo na wala hawatoulizana.”[1]

Katika Aayah nyingine amesema:

فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ

”Basi watakabiliana wenyewe kwa wenyewe wakiulizana.”[2]

Wanauliza ni vipi haya yatakuwa wazi. Hivyo wakaitilia shaka Qur-aan.

Kuhusu maneno Yake (´Azza wa Jall):

فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ فَلَا أَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلَا يَتَسَاءَلُونَ

”Wakati litakapopulizwa baragumu, basi hakutokuwa na unasaba baina yao Siku hiyo na wala hawatoulizana.”

hili litatokea pale kutapopulizwa baragumu kwa mara ya pili. Pindi watu wataposimama kutoka katika makaburi, basi hawatoulizana na wala hawatozungumza. Baada ya kufanyiwa hesabu na baadaye kuingia Peponi au Motoni, ndipo wataanza kusogeleana na kuulizana. Hii ndio tafsiri ya yale ambayo mazanadiki wameyatilia mashaka[3].

[1] 23:101

[2] 37:50

[3] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 64-65
  • Imechapishwa: 02/04/2024