Amesema:

وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا

”Tutawakusanya Siku ya Qiyaamah juu ya nyuso zao hali ya kuwa vipofu, mabubu na viziwi.”[1]

Amesema katika Aayah nyingine:

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ

”Watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi.”[2]

Vipi haya yatakuwa wazi wakati Anasema:

وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا

”Tutawakusanya Siku ya Qiyaamah juu ya nyuso zao hali ya kuwa vipofu, mabubu na viziwi.”

Kisha maeneo mengine anasema kuwa wataitana? Matokeo yake wakaitilia mashaka Qur-aan kwa sababu hiyo.

Ama kuhusu tafsiri ya Aayah:

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابَ النَّارِ

”Watu wa Peponi watawaita watu wa Motoni.”[3]

na:

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ

”Watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi.”,

ni pale mwanzoni watakapoingia Motoni watazungumza wao kwa wao. Wataita kwa sauti:

وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ

“Wataita: “Ee Maalik! Atumalize tufe Mola wako.” Atasema: “Hakika nyinyi ni wenye kubakia kuishi humo!”[4]

رَبَّنَا أَخِّرْنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ

”Mola wetu! Tuakhirishe mpaka muda mdogo… ”[5]

رَبَّنَا غَلَبَتْ عَلَيْنَا شِقْوَتُنَا وَكُنَّا قَوْمًا ضَالِّينَ

”Mola wetu! Matamanio yetu yalitutawala na tulikuwa watu waliopotea.”[6]

Watazungumza mpaka pale Atakapowaambia:

اخْسَئُوا فِيهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ

”Pateni utwevu humo! Na wala msinisemeshe!”[7]

Ndipo watakuwa vipofu, mabubu na viziwi. Utakoma usemi na kubaki kupumua kwa mngurumo na kuvuta pumzi kwa mkoromo. Hii ndio tafsiri ya yale ambayo mazanadiki wametilia shaka katika maneno ya Allaah[8].

[1] 17:97

[2] 7:50

[3] 7:44

[4] 43:77

[5] 14:44

[6] 23:106

[7] 23:108

[8] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 62-64
  • Imechapishwa: 02/04/2024