Amesema (´Azza wa Jall):

هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ

”Siku hii hawatotamka na wala hawatopewa idhini ili watoe nyudhuru zao.”[1]

Kisha akasema katika Aayah nyingine:

ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

”Halafu hakika nyinyi siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenu mtazozana.”[2]

Wanahoji ni vipi haya yatakuwa wazi. Aayah moja inasema:

هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ

”Siku hii hawatotamka… ”

Kisha Aayah nyingine inasema:

ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

”Halafu hakika nyinyi siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenu mtazozana.”

Wakadai kuwa maneno haya yanajigonga na hivyo wakaitilia mashaka Qur-aan:

Aayah:

هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ

”Siku hii hawatotamka na wala hawatopewa idhini ili watoe nyudhuru zao.”

inakusudia pale mwanzoni pindi watafufuliwa viumbe. Watanyamaza sawa na miaka sitini na hawatopata ruhusa ya kuomba udhuru. Baada ya hapo atawapa idhini ya kuzungumza, kama yanavyofahamisha maneno Yake (Ta´ala):

رَبَّنَا أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَارْجِعْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا

”Ee Mola wetu! Tumeshaona na tumeshasikia, hivyo basi turejeshe tufanye mema.”[3]

Pindi watapoidhinishwa kuzugumza, wataanza kuongea na kuzozana, kama ilivyo:

ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

”Halafu hakika nyinyi siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenu mtazozana.”

Bi maana wakati wa hesabu na  kulipiza kisasi. Halafu wataambiwa:

لَا تَخْتَصِمُوا لَدَيَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُم بِالْوَعِيدِ

”Msizozane Kwangu ilihali Nilishakutangulizieni Onyo Langu!”[4]

Kuanzia sasa hakuna jengine isipokuwa adhabu[5].

[1] 77:35-36

[2] 39:31

[3] 32:12

[4] 50:28

[5] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 02/04/2024