Upindaji wa mazanadiki juu ya zile Aayah zenye kutatiza

Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا

”Kila ngozi zao zitakapobanikika zikaungua Tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje adhabu. Hakika Allaah daima ni Mwenye nguvu Aliyeshinda, Mwenye hekima.”[1]

Mazanadiki wanasema:

”Ni kwa nini ngozi zao zilizoasi, na baadaye zikachomwa, zitabadilishwa kwa ngozi nyingine? Kwa maana nyingine ni kwamba Allaah ataziadhibu ngozi ambazo hazikutendea dhambi, kwa sababu Anasema:

بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا

”… Tutawabadilishia ngozi nyingine… ”

Wanaitilia shaka Qur-aan na kudai kuwa ni zenye kujigonga. Hapa ninasema kuwa maneno Yake Allaah (Ta´ala):

بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا

”… Tutawabadilishia ngozi nyingine… ”

si kwamba ni ngozi za mwengine. Kubadilishwa kwa ngozi hapa ni kuzifanya mpya. Kwa sababu ngozi zao zikishachomwa, Allaah atazifanya tena mpya. Qur-aan inayo [maandiko] maalum, yenye kuenea na njia nyingi na mawazo wanayoyatambua wanazuoni[2].

[1] 4:56

[2] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 02/04/2024