05. al-Ma´ribiy anawapa udhuru Ahl-ul-Bid´ah kwa kanuni iliyozuliwa

Tano ni kwamba unaona kuwa maneno ya watu ya ujumla yanatakiwa kufasiriwa kwa maneno yao yaliyopambanuliwa. Unatumia kanuni hii ili uweze kugeuza makoti yao kutegemea na upepo hata kama watakuwa wakweli. Tusemeje ikiwa maoni yao yameathirika kwa matamanio wanayoyaona? Unarekebisha kauli zao kwa kutumia kanuni hii.

Jambo la kufasiri yaliyo ya jumla kwa yaliyopambanuliwa linakuwa katika maneno ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu mtu ambaye hakukingwa wakati vitendo vyake vinatofautiana na yale anayoyasema, hilo linapelekea kukadhibishwa na pia kutiliwa shaka kwa sababu ya kutokuwa na msimamo. Vivyo hivyo pale ambapo maneno yake yanajigongagonga.

Mfano wa hilo ni kwamba Abul-Hasan anampa udhuru al-Maghraawiy na Sayyid Qutwub kwa makosa yao makubwa. Anadai kuwa maneno yao ya jumla yanatakiwa kufasiriwa kwa maneno yao yaliyopambanuliwa. Mwenendo huo unatia kasoro ´Aqiydah ya Abul-Hasan na ni dalili ya namna alivyoanguka na kuwatetea Ahl-ul-Bid´ah kwa nguvu zote Takfiyr zao, Wahdat-ul-Wujuud, kupindisha kwao sifa na mengine.

Akisema kuwa yeye ametubu juu ya makosa ishirini, ikiwa ni pamoja na nyudhuru kwa Sayyid Qutwub na al-Maghraawiy, kupitia kwa wanazuoni wa al-Madiynah basi tutamwambia yafuatayo:

1 – Umetubu juu ya Bid´ah ishirini na ukabakiza mengine. Moja wapo ni kanuni isemayo kwamba maneno ya watu ya ujumla yanatakiwa kufasiriwa kwa maneno yao yaliyopambanuliwa. Bado umeshikilia hili. Hili halunufaishi. Bado uko katika Bid´ah[1].

2 – Wakati ulipotoka al-Madiynah na ukapita kwa Shaykh Rabiy´ Makkah alikwambia kuwa bado uko na makosa mengine. Lakini ulikataa kusikiliza maneno yake na ukaondoka zako. Lau ingelikuwa umetubia tawbah ya kweli basi ungejirudi juu ya Bid´ah zako zote.

3 – Ulisafiri kwenda ar-Riyaadh na ukakutana na Ahl-ul-Bid´ah. Tulipata khabari hiyo kipindi hicho na ni jambo lililotusikitisha.

4 – Unatetea ”mfumo mpana”. Mfumo mpana huo kwa mujibu wako ni mfumo ambao unawapa nafasi makundi yote kukiwemo al-Ikhwaan al-Muslimuun, Qutbiyyuun, Jamaa´at-ut-Tabliygh, Salafiyyuun na wengineo. Mfumo huu ambao unawapa nafasi wale wenye haki na wenye makosa ni mfumo ambao umeuzua wewe mwenyewe. Wewe unasema kuwa ni Salafiy; iko wapi Salafiyyah yako?

Nadhani unaweza kufikiri kuwa mimi naacha yale mambo ya dhahiri na naingia ndani ya nia. Daima umeshikilia maudhui hayo ili Salafiyyah wasiwazungumzie Hizbiyyuun na kuwatuhumu Hizbiyyah kutokana na ushahidi. Wewe unataka kufuta hoja hizo. Hapa chini kunafuatia mapokezi kadhaa:

1 – al-Awzaa´iy amesema:

”Yeyote mwenye kutuficha Bid´ah yake basi hayatofichikana kwetu matangamano yake.”

Bi maana ikiwa matangamano yake ni Ahl-ul-Bid´ah basi na yeye anazingatiwa ni katika wao. Je, maimamu hawa wameenda kinyume na Qur-aan na Sunnah wakati walipohukumu matangamano haya ya kimadhambi yaliyo dhahiri?

2 – Sa´iyd al-Qattwaan amesema:

“Pindi Sufyaan ath-Thawriy alipofika Baswrah akaanza kuulizia juu ya ar-Rabiy´ bin Subayh na nafasi yake kwa watu. Akasema: “Ana I´tiqaad ipi?” Wakasema: “Hana I´tiqaad nyingine zaidi ya Sunnah.” Akasema: “Marafiki zake ni kina nani?” Wakasema: “Qadariyyah.” Ndipo akasema: “Basi na yeye ni Qadariy!”

3 – Fudhwayl bin ´Iyaadhw (Rahimahu Allaah) amesema:

“Roho ni wanajeshi walioshikana. Wale ambao wataafikiana wataungana na wale ambao hawatoafikiana watatengana. Mtu wa Sunnah hawezi kumnusuru mzushi isipokuwa kwa unafiki.”

4 – Ibn Battwah amesema:

”al-Awzaa´iy aliambiwa: ”Kuna mtu anasema kuwa yeye anachanganyika na Ahl-us-Sunnah na Ahl-ul-Bid´ah.” al-Awzaa´iy akasema: ”Mtu huyu anataka kulinganisha haki na batili.”

5 – Ibn-ul-Mubaarak amesema:

”Kaa na wale masikini na tahadhari kukaa na wazushi.”

6 – Mu´aadh bin Mu´aadh amesema:

”Nilisema kumwambia Yahyaa bin Sa´iyd: ”Hata  kama mtu atatuficha maoni yake basi hilo halitojificha kwa mwanawe, rafiki yake wala matangamano yake.”

7 – Muhammad bin ´Ubaydillaah al-Ghulaabiy amesema:

”Ilikuwa inasemwa kwamba Ahl-ul-Ahwaa´ wanaweza kuficha kila kitu isipokuwa matangamano na urafiki.”

Ee Abul-Hasan! Unaona kuwa elimu yako imebobea zaidi kuliko elimu ya maimamu hawa au kuwa una akili kubwa kuliko akili yao?

Ee Abul-Hasan! Unasemaje juu ya utetezi wako kwa wazushi hawa ambao wametumbikia ndani ya Bid´ah kubwa kama vile Bid´ah ya kuona kuwa kila kitu ni Allaah, ambayo ndio aina kubwa kabisa ya ukafiri, na kuwakufurisha kwao waislamu? al-Maghraawiy na Takfiyriyyuun wengine hawakuchukua Takfiyr zao isipokuwa kutoka katika vitabu vya Sayyid Qutwub. Yeye ndiye mwalimu wao katika jambo hilo.

[1] Shaykh Rabiy´ (Hafidhwahu Allaah) amesema:

”Wakati alipoulizwa juu ya Bid´ah hizi ishirini akasema: ”Si sahihi. Nimejirejea tu mambo mawili ambayo tayari nimekwishajirejea nayo huko Yemen.”

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tanbiyh al-Wafiy ´alaa Mukhaalafaat Abiyl-Hasan al-Ma’ribiy, uk. 294-302
  • Imechapishwa: 03/12/2022