Uniangalie pamoja na wale Unaowaangalia – Kwa maana ya kwamba kuwa ni Mlinzi wetu. Kuna aina mbili ya ulinzi (الولاية):

1 – Ulinzi wenye kuenea.

2 – Ulinzi maalum.

Ulinzi maalum unakuwa kwa waumini. Kama alivosema Allaah (Ta´ala):

اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ

“Allaah ni mlinzi wa wale ambao wameamini; Anawatoa kutoka katika viza na  kuwaingiza katika nuru.  Na wale ambao wamekufuru walinzi  wao ni Twaaghuut.”[1]

Kwa hivyo unamwomba Allaah ulinzi maalum ambao unapelekea utunzaji kwa yule ambaye Allaah (´Azza wa Jall) anamwangalia na kumuwafikisha katika yale anayoyapenda na kuyaridhia.

Lakini ulinzi wenye kuenea anaingia kila mmoja. Allaah ni mlinzi wa kila mmoja. Kama alivosema Allaah (Ta´ala):

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ

”… mpaka kinapomfikia mmoja wenu kifo, basi wajumbe Wetu humfisha, nao hawazembei.”[2]

Hili ni lenye kuenea kwa kila mmoja. Kisha akasema:

ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ

”Kisha watarudishwa (wote waliofishwa) kwa Allaah Rabb wao wa haki.”[3]

Lakini wakati tunaomba kwa kusema:

اللهم اجعلنا من أوليائك

”Ee Allaah! Tujaalie kuwa katika wapenzi Wako.”

اللهم تولنا

”Ee Allaah! Tulinde.”

tunakusudia ulinzi maalum ambao unapelekea kutiliwa manani na kuwafikishwa katika yale anayopenda na kuyaridhia.

[1] 02:257

[2] 06:61

[3] 06:62

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 09-10
  • Imechapishwa: 09/03/2024