Uniafu pamoja na wale Uliowaafu – Tuponye kutokana na maradhi ya mioyo na maradhi ya miili. Ndugu! Unatakiwa kuhudhurisha moyo na huku unaomba du´aa ya kwamba akusalimishe kutokana na magonjwa ya mwili na maradhi ya moyo, kwa sababu maradhi ya moyo ni makubwa zaidi kuliko maradhi ya mwili. Ndio maana tunasema katika du´aa ya Qunuut:

اللهم لا تجعل مصيبتنا في ديننا

”Ee Allaah! Usifanye msiba wetu katika dini yetu.”

Magonjwa ya mwili yanatambulika. Lakini magonjwa ya moyo yanarejea katika mambo mawili:

1 – Magonjwa ya tamaa ambayo chanzo chake ni matamanio.

2 – Magonjwa ya shubuha ambayo chanzo chake ni ujinga.

1 – Magonjwa ya tamaa ambayo chimbuko lake ni matamanio mtu akaitambua haki, lakini asiitake. Kwa sababu mtu huyu yuko na matamanio ambayo yanaenda kinyume na yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

2 – Magonjwa ya shubuha ambayo chimbuko lake ni ujinga. Kwa sababu mjinga hufanya batili na huku akadhani kuwa ni haki. Maradhi haya ni khatari mno.

Kwa hivyo wewe unamuomba Allaah akusalimishe usalama kutokana na maradhi ya miili na maradhi ya mioyo ambayo ni yale magonjwa ya shubuha na matamanio.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 08-09
  • Imechapishwa: 09/03/2024