04. Ummah ni wenye kuhitaji sana kulinganiwa

Maimamu wa uongofu ambao ni wanafunzi wa Maswahabah na wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah– waarabu na wasiokuwa waarabu – wakawafuata katika mfumo huu. Walifuata mfumo huu ambao ni wa kulingania katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall), wakabeba migizo yake na wakatekeleza amana yake pamoja na ukweli, subira, kumtakasia nia Allaah katika kupambana katika njia Yake, kumpiga vita anayetoka nje ya dini Yake na kuzuilia kutokamana na njia Yake baada ya kukataa kulipa kodi iliyofaradhishwa na Allaah wakiwa wanatakiwa kufanya hivo. Wao ndio wabebaji wa Da´wah na viongozi wa uongofu baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vivyo hivyo wafuasi wa Maswahabah ambao ni wanafunzi wa Maswahabah na wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah na maimamu wa uongofu. Wote hao walipita juu ya mfumo huu kama tulivyotangulia kusema. Wakasubiri juu ya hayo, ikasambaa dini ya Allaah, neno Lake likawa juu kupitia mikono ya Maswahabah na wale wanazuoni na waumini waliowafuata ambao walikuwa waarabu na wasiokuwa waarabu kutoka katika kisiwa hiki kuanzia kusini na kaskazini mwake. Walikuweko wengine wanaotoka nje ya kisiwa katika pande mbalimbali za ulimwengu miongoni mwa wale ambao Allaahamewaandikia furaha, wakaingia ndani ya dini yaAllaah, wakashiriki katika kulingania na kupambana, wakasubiri juu ya hayo na wakawa na ufalme na uongozi katika dini. Yote hayo kutokana na subira, imani na kupambana kwao katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Maneno Yake (Subhaanah) aliyoyataja juu ya wana wa israaiyl yakasadikika juu yao:

وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ

”Na Tukawafanya miongoni mwao waongozi wanaoongoa watu kwa amri Yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na ishara zetu.”[1]

Haya yalisadikika juu ya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale waliofuata mfumo wao. Walikuwa viongozi, wenye kuongoza, walinganizi wa haki na wanazuoni wanaoigilizwa. Hilo ni kutokana na subira na imani yao. Kwa subira na yakini ndio mtu anapata uongozi katika dini. Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale waliowafuata kwa wema mpaka hii leo ndio viongozi, wenye kuongoza na ndio viongozi katika njia ya haki.

Kwa hivyo inapata kumbainikia kila mwanafunzi ya kwamba kulingania kwa Allaah ni miongoni mwa mambo muhimu kabisa na kwamba Ummah katika kila zama na kila mahali wanahitaji hilo sana. Bali ni wenye dharurah kubwa juu ya jambo hilo.

[1] 32:24

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 31/05/2023