04. Picha – inachukiza au ni haramu?

Suala la pili: Baada ya kusihi kwa katazo, je, linakusudia kuwa ni haramu au inachukiza?

Tayari tumethibitisha hapo awali kuwa dalili zinazoonyesha kwamba mtengeneza picha ataadhibiwa Motoni zinajulisha uharamu kwa namna iliyo wazi zaidi kuliko dalili za katazo tu. Kwa hiyo kutengeneza picha za viumbe hai ni haramu. Ufafanuzi wake ni kwamba mtengeneza picha ametishiwa na Mwekaji Shari´ah kuwa ataadhibiwa Motoni. Kila ambaye Mwekaji Shari´ah amemtishia kuwa ataadhibiwa Motoni ni mtendaji wa jambo lililoharamishwa. Kwa msemo mwingine mtengeneza picha ni mtendaji wa jambo lililoharamishwa. Ama dalili ndogo ni Hadiyth sahihi zilizotajwa hapo awali. Katika Shari´ah ya Kiislamu ni jambo linalotambulika vyema kwamba mtu hatishiwi kwa kuacha jambo linalopendeza au kwa kufanya jambo linalochukiza. Wala kwa kufanya jambo lililoruhusiwa au kuliacha. Hivyo basi hakubaki isipokuwa kufanya jambo lililoharamishwa au kuacha wajibu. Kutengeneza picha ni katika kufanya jambo lililoharamishwa na hivyo kutengeneza picha ikawa ni haramu.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin ´Aliy ash-Shawkaaniy (afk. 1250)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm-ut-Taswwiyr, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 06/05/2026