04. Njia pekee ya kuwafanya waislamu kuwa na umoja

Hii ndio inakuwa natija ya mwisho. Kila ambaye hachukui dini na ´Aqiydah yake kutoka katika Qur-aan na Sunnah, basi natija ya mwisho inakuwa ni mfarakano na tofauti. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

“Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja Nami ni Mola wenu, basi Nicheni. Lakini wakalivunja jambo lao baina yao makundi mbalimbali, kila kundi kwa waliyokuwa nayo linafurahia.” (23:52-53)

Kila mmoja akazua madhehebu na mfumo wenye kutofautiana na mwengine. Matokeo yake kukatokea fitina na shari kubwa. Hakuna njia nyingine ya kuyaepuka isipokuwa kwa kushikamana na Qur-aan na Sunnah na khaswa inapokuja katika jambo la msingi ambalo ni ´Aqiydah. Allaah huwafanya watu wakawa na umoja kupitia ´Aqiydah. Amesema (Ta´ala):

وَإِن يُرِيدُوا أَن يَخْدَعُوكَ فَإِنَّ حَسْبَكَ اللَّـهُ ۚ هُوَ الَّذِي أَيَّدَكَ بِنَصْرِهِ وَبِالْمُؤْمِنِينَ وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ ۚ لَوْ أَنفَقْتَ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مَّا أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

“Wakitaka kukuhadaa, basi Allaah anakutosheleza. Hakika Yeye ndiye ambaye amekusaidia kwa nusura Yake na kwa waumini na Akaunganisha nyoyo zao. Lau ungelitoa vyote vilivyomo ardhini, basi usingeliweza kuunganisha nyoyo zao lakini Allaah amewaunganisha. Hakika Yeye ni Mwenye nguvu Aliyeshinda, Mwenye hekima.” (08:62-63)

Vijizawadi na mali nyingi hazifanyi nyoyo zikawa na umoja. Kinyume chake mambo haya yanazidisha chuki. Vovyote utavyotoa mali zako huwezi kuzifanya nyoyo zikawa na umoja. Kinachofanya nyoyo zikawa na umoja ni Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 16/12/2023