Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hii ndio dini ya Mitume ambayo Allaah amewatuma kwayo kwa waja Wake.

MAELEZO

Shaykh (Rahimahu Allaah) anamaanisha Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ya kwamba ndio dini ya Mitume. Wote walitumwa kwa ajili ya msingi huu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuut [miungu ya uongo].”” (16:36)

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi; hivyo basi niabuduni.”” (21:25)

Washirikina ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapiga vita walipotea kwa aina hii ya Tawhiyd. Hivyo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akahalalisha damu, mali, ardhi na nyumba zao. Vilevile wanawake wao wakafanywa wajakazi.

Mwenye kuharibu aina hii ya Tawhiyd ni mshirikina na kafiri, haijalishi kitu hata kama atatambua Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat.

Kumpwekesha Allaah pekee kwa ´ibaadah ndio dini ambayo Allaah kawatuma Mitume kwayo kwa waja Wake, kama ambavyo alivyosema Shaykh (Rahimahu Allaah). Allaah ameeleza kuwa Mtume wa kwanza ni Nuuh (´alayhis-Salaam) amesema:

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ أَن لَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ

“Hakika Tulimtuma Nuuh kwa watu wake [akawaambia]: “Hakika mimi kwenu ni mwonyaji wa wazi, ya kwamba msiabudu mwengine isipokuwa Allaah.”” (11:25-26)

Amesema (Ta´ala):

وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ

“Na kwa kina ‘Aad [Tulimpeleka] ndugu yao Huud. Akasema: “Ee watu wangu! Mwabuduni Allaah, kwani hamna mungu wa haki mwengine asiyekuwa Yeye.”” (11:50)

وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ

“Na kwa [watu wa] Madyan [Tulimpeleka] ndugu yao Shu’ayb. Akasema: “Enyi watu wangu! Mwabuduni Allaah, kwani hamna mungu wa haki asiyekuwa Yeye.”” (11:84)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Utaymiyn
  • Mfasiri: Fitqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 23/04/2022