Suala la nne ni kusubiri juu ya maudhi yatayompata mtu ndani yake. Mtu anaweza kusibiwa na maudhi. Anaweza kuudhiwa na wale anaowalingania, familia yake au wengine. Kwa hivyo ni wajibu kuwa na subira na kutaraji malipo kutoka kwa Allaah. Muumini anakuwa na subira kwa kumuamini Allaah, kutendea kazi yale Allaah aliyomuwajibishia na kumuharamishia, kulingania katika dini ya Allaah, mafundisho na kuamrisha mema na kukataza maovu. Yote haya yanahitajia subira. Dini yote inahitajia subira. Kulingania katika dini ya Allaah, kuswali, kutoa zakaah, kufunga, kuhiji, kuamrisha mema, kukataza maovu na kujiepusha kabisa na vile vilivyoharamishwa, yote yanahitajia subira. Mtu asipokuwa na subira hutumbukia katika yale Allaah aliyoharamisha au huacha yale Allaah aliyomuwajibishia. Kwa ajili hii ndio maana Allaah (Ta´ala) amesema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ

“Basi subiri kama walivyosubiri wenye azimio madhubuti katika Mitume.” (46:35)

وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ

“Subiri hukumu ya Mola wako.” (52:48)

وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِاللَّـهِ

“Subiri [kumbuka kuwa] haiwi kusubiri kwako isipokuwa kupitia kwa Allaah.” (16:127)

إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ

“Hakika wale wanaosubiri watalipwa ujira wao bila ya hesabu.” (39:10)

وَاصْبِرُوا ۚإِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ

“Subirini! Hakika Allaah yu pamoja na wale wenye kusubiri.” (08:46)

Bi maana kuwa na subira katika kumtii Allaah na jiepushe na makatazo Yake. Tahadharini kwenda kinyume na maamrisho Yake na kutekeleza makatazo Yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 08-09
  • Imechapishwa: 15/10/2016