Suala la tatu ni kuilingania. Unachotakiwa ni wewe kulingania katika dini hii na uwanasihi watu wawe na msimamo juu yake. Unatakiwa kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu. Huku ndio kulingania katika dini ya Allaah. Ni lazima kwa kila muislamu kulingania katika dini ya Allaah kiasi na uwezo wake. Kila mmoja, mwanaume na mwanamke, ni wajibu kwake kulingania, kufikisha, kuelekeza na kunasihi kwa njia moja au nyingine. Wanatakiwa wawaamrishe watu kumuabudu Allaah peke yake, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan, kuhiji Nyumba kwa kuwepo uwezo, kuwatendea wema wazazi, kuwaunga ndugu na kujiepusha na madhambi yote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 08
  • Imechapishwa: 15/10/2016