Suala la pili ni kuifanyia kazi. Bi maana kutendea kazi matendo ya dini hii kama swalah, swawm, Jihaad, hajj, imani na uchaji Allaah. Unatakiwa kuutendea kazi Uislamu kwa sababu wewe umeumbwa kwa ajili yake. Umeumbwa kwa ajili ya kumuabudu Allaah. Ni wajibu kwako kujifunza dini ya Allaah na kuitendea kazi. Unatakiwa umuabudu Allaah peke yake, uswali, utoe zakaah, ufunge Ramadhaan na uwende kuhiji kwenye Nyumba. Unatakiwa kumuamini Allaah, Malaika wake, Vitabu vyake, Qiyaamah na Qadar kheri na shari yake. Unatakiwa kuamrisha mema, kukataza maovu, kuwatendea wema wazazi wako, kuwaunga ndugu zako na mengineyo. Unatakiwa kuyafanya yale Allaah aliyokuamrisha na ujiepushe na yale aliyokukataza. Unatakiwa kufanya ya wajibu ambayo wewe umewajibishwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 08
  • Imechapishwa: 15/10/2016