04. Kuacha swalah ni ukafiri, upotofu na kutoka nje ya Uislamu

Inatambulika kwamba kuacha kuswali ni ukafiri, upotofu na kutoka nje ya mzunguko wa Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Baina ya mtu na shirki na ukafiri ni kuacha swalah.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh).

 Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule atakayeiacha amekufuru.”[2]

Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa nne wa Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Aayah na Hadiyth juu kutukuza jambo la swalah, ulazima wa kuichunga, kuisimamisha kama alivoiweka Allaah katika Shari´ah na matahadharisho ya kuiacha ni nyingi na zinazotambulika. Kwa hivo ni lazima kwa kila muislamu kuihifadhi ndani ya wakati wake, aisimamishe kama alivoiweka Allaah katika Shari´ah na aiswali ndani ya nyumba za Allaah pamoja na ndugu zake. Afanye hivo hali ya kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutahadhari na ghadhabu za Allaah na adhabu Yake kali.

Pindi haki itapodhihiri na zikabainika dalili zake haitofaa kwa yeyote kuiacha kutokana na maoni ya fulani. Allaah (Subhaanah) amesema:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[3]

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake; isije kuwapata fitina au ikawapata adhabu iumizayo.”[4]

[1] Muslim (82).

[2] Ahmad (21859) na at-Tirmidhiy (2545).

[3] 04:59

[4] 24:63

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 16/11/2021