03. Moja katika sababu kubwa za kuacha swalah kabisa

Kwa hiyo ni lazima kwa kila muislamu kutilia umuhimu jambo hili, kulikimbilia na kushauriana pamoja na watoto wake, watu wa nyumbani kwake, majirani zake na ndugu zake wengine waislamu. Wafanye hivo kwa ajili ya kutekeleza amri ya Allaah na Mtume Wake na kutahadhari kutokamana na yale aliyokayaza Allaah na Mtume Wake na kujiepusha kujifananisha na wanafiki ambao Allaah amewasifu kwa sifa mbaya ambayo mbaya zaidi katika hizo ni kuifanyia uvivu swalah. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا مُّذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَٰلِكَ لَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ وَلَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا

“Hakika wanafiki wanafikiri wanamhadaa Allaah na hali Yeye ndiye Mwenye kuwahadaa na wanaposimama kuswali basi husimama kwa uvivu, wakijionyesha kwa watu na wala hawamtaji Allaah isipokuwa kidogo tu. Wenye kuyumbayumba kati ya hayo, huku hawako wala huko hawako. Na ambaye Allaah amempotoa huwezi kumpatia njia [ya yeye kuongoka]”[1]

Kuacha kuswali msikitini katika mkusanyiko ni miongoni mwa sababu kubwa za kuiacha kabisa.

[1] 04:142-143

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 15
  • Imechapishwa: 16/11/2021