04. Jukumu la wahubiri siku ya ijumaa

Ni lazima kwa waislamu waitilie umuhimu na waichunge pamoja na zile swalah zengine tano zilizobaki ili afaidike na yale ambayo Allaah ameweka Shari´ah ndani yake na akumbuke zile kheri tukufu ambazo Allaah amepanga juu ya mkusanyiko ikiwa ni pamoja na kujuana, kuwasiliana, kusaidiana katika wema na kumcha Allaah, kusikiliza mawaidha, Khutbah na kuathirika kwa mambo hayo pamoja na yale yanayopelekea katika jambo hilo katika kheri nyingi na ujira mkubwa kukiwemo kuamrishana mema, kukatazana maovu, baadhi kuwatembelea wengine, kunasihiana, kusaidiana kuanzisha miradi ya hisani na kujua yale mambo ya Uislamu yanayoweza kuwa yenye kujificha kwao na khaswa pale ambapo wahubiri wataipa umuhimu Khutbah na wakaipa yale maandalizi inayohitajia na kutilia umuhimu yale mambo muhimu ya watu katika mambo ya dini na dunia yao. Hivo ndivo walivyozindua wanazuoni. Hakika muhubiri analo jukumu kubwa. Aipe umuhimu Khutbah mpaka mpaka ndugu zake wabainikiwe na zile hukumu za Allaah ambazo zinaweza kuwa zimefichikana kwao. Hivyo kila Khutbah ndani yake kunakuwa na maelekezo na miongozo. Aidha awatambuze zile hukumu ambazo zinaweza kuwa zimefichikana kwa watu, kuwakumbusha yale ambayo Allaah amewawajibishia, yale ambayo Allaah amewaharamishia, kuwakumbusha na kile ambacho Allaah amewakataza na mengineyo ambayo muhubiri anaona kuwa ni vizuri kuwalekeza na kuwaongoza kwayo na khaswa matatizo ya sasa na zile hukumu zinazoweza kujificha kwao.

Miongoni mwa watu wako ambao ni wajinga, walioghafilika na wajuzi. Wajuzi inazidi elimi yao na wanajikumbusha yale ambayo yanaweza kuwa yamefichikana kwao. Watu wengine wanakumbuka na wajinga wanajifunza. Kwa hivyo faida inakuwa yenye kuwaenea watu wote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 30/11/2021