271 – Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن حَفَر ماءً لم يَشْرَبْ منه كبِدٌ حرّى من جِن، ولا إنسٍ، ولا طائرٍ؛ إلا آجرَه الله يومَ القيامةِ، ومَن بنى مسجداً كمَفْحص قَطاةٍ أو أصغرَ؛ بنى الله له بيْتاً في الجنةِ

“Yeyote atakayechimba kisima ambapo majini, watu na ndege wenye kiu wakanywa humo, basi Allaah atamlipa ujira siku ya Qiyaamah. Yeyote atakayejenga msikiti kiasi cha fuko la ndege au mdogo zaidi, basi Allaah atamjengea nyumba Peponi.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh”. Ibn Maajah ametaja kujenga msikiti peke yake, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/228)
  • Imechapishwa: 09/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy