04. Hadiyth ”Muadhini anasamehewa kwa umbali inapofikia sauti yake… “

234 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´an) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

المؤذنُ يُغفَر له مدى صوتِهِ، ويُصَدِّقُه كلُّ رطْبٍ ويابسٍ

”Muadhini anasamehewa kwa umbali inapofikia sauti yake. Kinamsadikisha kila kilichorutubika na kikavu.”[1]

Ameipokea Ahmad na tamko ni lake, Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake. Imekuja kwa wawili hao:

“Kinamtolea ushuhuda kila kilichorutubika na kikavu.”

Kwa an- Nasaa´iy kuna nyongeza isemayo:

“Aidha analipwa ujira kiasi cha kila ambaye ataswali pamoja naye.”[2]

Imekuja kwa Ibn Maajah:

“Anasamehewa kwa umbali inapofikia sauti yake. Kinamuombea msamaha kila kilichorutubika na kikavu. Kinamuombea msamaha kila kilichorutubika na kikavu.”[3]

Ibn Hibbaan amepokea katika “as-Swahiyh” yake:

”Muadhini anasamehewa kwa umbali inapofikia sauti yake. Kinamuombea msamaha kila kilichorutubika na kikavu. Anayeshuhudia swalah anaandikiwa thawabu ishirini na tano[4] na anasamehewa yaliyo kati yake.”[5]

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Swahiyh. Hata hivyo Hadiyth hii imepokelewa na al-Baraa´ na sio Abu Hurayrah.

[3] Nzuri na Swahiyh.

[4] Bi maana yule anayeshuhudia swalah ya mkusanayiko kwa adhaana aliotoa.

[5] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/213-214)
  • Imechapishwa: 22/02/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy