04. Dalili ya tatu juu ya kufaradhishwa kufunga Ramadhaan

3 – Imethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunga ´Aashuuraa´ na akaamrisha kuifunga. Wakati kulipofaradhishwa Ramadhaan ikaachwa.”[1]

Maneno yake:

“… ikaachwa.”

Bi maana ikaachwa swawm ya ´Aashuuraa´ hali ya kuwa lazima na kukabakia kule kupendezwa kwake. Haafidh Ibn Hajar amesema:

“Hakukuachwa kule kupendekezwa kwake. Ni kitu kilichobakia. Ikafahamisha kuwa kilichoachwa ni ule ulazima wake.”[2]

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia:

“Quraysh walikuwa wakifunga siku ya ´Aashuuraa´ kabla ya kuja Uislamu. Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha kuifunga mpaka ilipofaradhishwa Ramadhaan. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Mwenye kutaka kuifunga aifunge na mwenye kutaka ale.”[3]

[1] al-Bukhaariy (1892).

[2] Fath-ul-Baariy (04/237).

[3] al-Bukhaariy (1893) na Muslim (1125).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ilmaam bishay´ min Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 11
  • Imechapishwa: 26/03/2023