04. al-Ma´ribiy anawaita Salafiyyuun kuwa ni ”Haddaadiyyah”

Nne ni kwamba umewatuhumu Salafiyyuun ambao wamekukemea maneno yako juu ya Maswahabah kwamba ni takataka za mafuriko na mengineyo na wakakuomba urejee katika haki – lakini ukakataa na ukaendelea kung´ang´ania – kwamba ni Haddaadiyyah. Udhahiri wa Haddaadiyyah ni kwamba wanakufurisha kwa Bid´ah moja peke yake. Wanasema kuwa ni lazima kwetu kutomuombea rehema yule mwanachuoni anayetumbukia kwenye Bid´ah moja tu na kwamba haifai kwetu kusoma vitabu vyao. Bali wanasema kuwa ni lazima pia kuchoma moto vitabu vyake. Wamekubali wenyewe kwamba wametia moto ”Fath-ul-Baariy”.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tanbiyh al-Wafiy ´alaa Mukhaalafaat Abiyl-Hasan al-Ma’ribiy, uk. 292-294
  • Imechapishwa: 02/12/2022