Tatu ni kwamba umewaeleza Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba ni ”takataka za mafuriko” (غثائية)[1]. Hili linajulisha uchache wako wa kuwafanyia adabu. Vivyo hivyo maneno yako uliyosema kuhusu Usaamah bin Zayd (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipomuua yule bwana ambaye baadaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkaripia[2].

[1] al-Ma´ribiy amesema:

”Katika hali kama hiyo kulingania kwa Allaah kunatakiwa kuwe kwa miisngi na tahadhari kutokamana na takataka. Takataka ilikuweje siku ya Hunayn? Takataka ilikuweje siku ya Hunayn? Wema na wakweli walifichuka mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo kamwe huwezi kujiaminisha kutokana na talakataka. Takataka ni shari kubwa.” (Kanda ”al-Fahm as-Swahiyh li ba´dhw Usuwl-is-Salafiyyah”)

[2] al-Ma´ribiy amesema:

”Usaamah alisema: ”Naapa kwa Allaah amesema hivo kwa sababu ya woga.” Tazama! Tazama namna Usaamah anavyochukuliwa na hisia! Amefikia mpaka kuapa juu ya hilo!” (Kaseti ”Raf´-ul-Hijaab”)

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Umefungua kifua chake ili uone kuwa amesema hivo kutokana na woga?” Ndipo Usaamah akaona kuwa hoja yake ilikuwa dhaifu na haikuwa na maana yoyote katika hali hii. Hali hii iko wazi kwa yule anayefata misingi na anayepelekwa na matamanio.” (Kaseti ”Raf´-ul-Hijaab”)

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tanbiyh al-Wafiy ´alaa Mukhaalafaat Abiyl-Hasan al-Ma’ribiy, uk. 291-292
  • Imechapishwa: 02/12/2022