04. Aina ya kwanza ya watu kuipokea Ramadhaan

Muislamu anatakiwa kufanya vizuri kuipokea Ramadhaan. Watu wanatofautiana kiasi kikubwa katika namna ya wanavopokea mwezi wa Ramadhaan.

1 – Kuna kundi la watu wanapokea mwezi huu kwa kukimbilia masokoni kwelikweli ili wanunue aina mbalimbali ya vyakula. Kwa hiyo utawaona wanashindana masokoni na wananunua aina mbalimbali ya vyakula kwa viwango vikubwa. Ni kana kwamba wanaupokea kwezi wa kula na kunywa. Hivyo wananunua ununuzi wenye kuzidi. Kiasi cha kwamba jambo la kwenda masokoni na ununuzi wa vyakula unazidi ndani ya Ramadhaan kutoka katika familia nyingi juu ya mahitaji yao. Kwa ajili hiyo, na khaswa wale watu wenye kufanya israfu, utawaona wanafanya ubadhirifu wa fedha na wanaweka aina nyingi za vyakula kwenye meza aina nyingi ya vyakula. Kisha hali kutoka katika vyakula hivyo isipokuwa kichache tu. Hili ni sampuli moja ya watu.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 08
  • Imechapishwa: 04/04/2022