05. Aina ya pili ya watu kuipokea Ramadhaan

2 – Aina nyingine ya watu unapofika Ramadhaan basi wanajiandalia zana za michezo, zana za pumbao na zana za kupoteza wakati. Vilevile wanajitayarishia mambo yatayoshughulisha nyakati zao zenye thamani ndani ya mwezi wa Ramadhaan katika kupoteza, kubadhirisha na kupoteza wakati katika mambo yasiyokuwa na faida. Bali mara nyingi katika mambo yaliyo na madhara yenye kuhakikiwa. Wanaiandalia Ramadhaan katika mfano wa mambo haya na wanajiandaa kikamilifu kabla ya kufika Ramadhaan.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 08-09
  • Imechapishwa: 04/04/2022