Neno hili la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) linazitikisa nyoyo ili waweze kuhisi thamani ya mwezi huu, nafasi yake na ngazi yake kubwa. Kwa msemo mwingine ni kama anasema jiandaeni nao, mjiandae kwa ujio wake, muupokee kwa mapokezi mazuri na ukirimuni kama anavokirimiwa mgeni.

Kikawaida watu hupeana bishara wao kwa wao kwa kufika mambo muhimu na mambo matukufu ili wajiandae na wawe tayari juu ya mambo hayo. Mwezi wa Ramadhaan ni mgeni mtukufu juu ya nafsi ya kila muumini. Kila muumini hufurahi furaha kubwa kwa mgeni huu aliyemfikia. Je, umemwona mtu ambaye ni mkarimu anayeburudika kwa ukarimu na kutoa anavokuwa pindi anapofikiwa na mgeni mtukufu na mwenye hadhi – ni vipi kunakuwa kumpokea kwake na namna anavyomfurahikia?

Maneno yake:

“Umekujieni mwezi wa Ramadhaan.”

Kwa msemo mwingine anachotaka kusema ni kwamba jiandaeni kumpokea mgeni huu mtukufu, jiandaeni kumkirimu na kumtekelezea haki yake na ziandaeni nafsi zenu juu ya hilo. Kwa sababu kama ambavo unakuja kwa haraka pia unaondoka kwa haraka. Kwa hivyo jiandaeni kwa ajili yake. Ziandaeni nafsi zenu kufanya matendo matukufu, matendo mazuri na ´ibaadah ambazo zinakufurahisheni kukutana na Mola wenu (Tabaarak wa Ta´ala) mkiwa nazo.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 07
  • Imechapishwa: 04/04/2022