Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kisha akaingia katika makusudio na akafungua kwa mtindo wa amri:

“Tambua”

kwa ajili ya kufahamisha angalizo na kufanya maandalizi juu ya kile anachotaka kukitoa kwa msikilizaji na msomaji baada ya neno “Tambua”. Kwa sababu haelewi maneno na kuelewa kile kinachotolewa isipokuwa ambaye amezinduka, ameamka, amelikusanya jambo lake na akalitega sikio lake. Huyu ndiye anafahamu vyema kile kinachosemwa katika maelekezo, upambanuzi wa maneno, ubainifu wa yaliyo halali na yaliyo haramu, akasikiliza mawaidha ima kwa kusikiliza au kwa kupiga simu. Kisha baada ya hapo akafuata uzindushi wa walinganizi wa kila msomaji na kila msikilizaji. Hii ndio njia miongoni mwa njia za wanachuoni ambao wanalipa umuhimu jambo la Uislamu na waislamu na wanapenda kheri kwa yule mwenye kuitafuta.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Twariyqal-Usuwl ilaa idhwaah-ith-Thalaat-il-Usuwl, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 17/11/2021