Ibn Baaz kuhusu Swalaat-ul-Tasbiyh

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya Tasaabiyh?

Jibu: Wanazuoni wametofautiana kuhusu Hadiyth ya swalah ya Tasaabiyh. Maoni ya sawa ni kwamba si Swahiyh. Ni yenye kupingana na Hadiyth ambazo ni Swahiyh na matini yake ni yenye munkari. Ni yenye kwenda kinyume na Hadiyth Swahiyh zinazotambulika kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah iliyopendekezwa. Nakusudia ile swalah ambayo Allaah amewawekea Shari´ah waja Wake katika Rukuu´, Sujuud yake na vyenginevyo. Kwa ajili hiyo maoni ya sawa ni yale maoni ya waliosema kuwa haikusihi kutokana na tuliyotaja. Jengine ni kwamba cheni za wapokezi wake zote ni dhaifu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/426)
  • Imechapishwa: 17/11/2021